Hotline: (+255) 24-2230271 Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 

Sub Page Name

×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 305

Proin sed odio et ante adipiscing lobortis Proin sed odio et ante adipiscing lobortis

Mageuzi na Mikakati Yametimiza Azma ya Serikali Kuimarisha Sekta ya Karafuu

  • Written by 
  • Tagged under Lorem
  • Wednesday, 18 July 2012 00:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema mageuzi yaliyofanywa katika Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ZSTC chini ya Sheria Mpya ya ZSTC namba 11 ya mwaka 2011, Sheria ya Maendeleo ya Karafuu namba 2 ya mwaka 2014 na Mkakati wa miaka kumi (2011/2021) wa Mageuzi katika Sekta ya Karafuu yametimiza lengo la Serikali la kuliimarisha zao la karafuu.

Akizungumza na uongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko na Shirika la ZSTC Ikulu Mjini Zanzibar, Dkt. Shein amesema mambo hayo ya msingi yaliyofanywa na Serikali kwenye Sekta ya Karafuu na Shirika la ZSTC ni mfano kwa taasisi nyengine katika kufanya mageuzi ya maendeleo.

Alifahamisha kwa kipindi chote cha miaka sita cha mageuzi yaliyoanza mwaka 2011, bei ya karafuu kwa wakulima imekuwa nzuri na ya uhakika ambapo wakulima wanalipwa wastani wa TZS 14,000 na Serikali haijaona sababu ya kushusha bei hiyo.

Alisema Serikali kupitia Shirika la ZSTC imeimarisha zaidi huduma kwa wakulima ikiwemo ujenzi wa vituo vya ununuzi vya kisasa vyenye hadhi ambapo jumla ya vituo vyote Unguja na Pemba ni 32.  Vituo hivyo vina huduma zote za msingi kwa matumizi ya wakulima wa zao la karafuu.

Alibainisha kuwa mikopo kwa wakulima inayotolewa bila ya riba na miche ya mikarafuu ambayo huzalishwa na kutolewa kwa wakulima bila ya malipo na elimu juu ya uimarishaji wa zao hilo ni juhudi maalum za kuliendeleza zao hilo la karafuu.

Alisema ili kuendelea kuwaenzi wakulima wa zao la karafuu na kuhakikisha wanauza karafuu zao serikalini bila ya shida Serikali inatekeleza mpango wa ujenzi wa miundombinu ya barabara katika maeneo yenye karafuu nyingi ili kuwarahisishia wakulima kuleta karafuu zao katika vituo vya ununuzi na kuona faida ya juhudi zao za uimarishaji wa zao hilo.

Alisema Serikali itafanya kila juhudi katika kuliimarisha zao la karafuu na wala haitosita kufanya mabadiliko yoyote ya sheria yatakayoleta manufaa kwa wakulima wa zao hilo na sekta nzima ya karafuu.

Aidha, aliitaka Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa Shirika la ZSTC kuzisoma na kuzifahamu vyema Sheria zinazoongoza Sekta ya karafuu ili kutekeleza vyema majukumu ya uendelezaji wa zao la karafuu na kutosita kupeleka mapendekezo serikalini juu ya mabadiliko ya Sheria endapo wakiona ipo haja ya kufanya hivyo.

Awali akitoa maelezo kwa Rais, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la ZSTC Dkt. Said Seif Mzee alisema katika utekelezaji wa mageuzi Shirika limejizatiti katika uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na la nje.

Alifahamisha kuwa soko la mazao ya kilimo na viwandani kutoka Zanzibar ni kubwa nchi za nje ambapo linatoa changamoto kwa Shirika na wakulima kuzalisha mazao mengi zaidi na yenye ubora ili kukidhi mahitaji ya soko hilo.

Alisema kuwa Shirika la ZSTC limepanga kufanya mageuzi makubwa katika kiwanda cha uzalishaji wa mafuta ya mimea na makonyo kilichopo Wawi Chake chake Pemba ili kuongeza uzalishaji kufuatia mahitaji makubwa ya bidhaa hizo katika soko la China, Uingereza na Pakistan.

Nae Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali alisema kuna umuhimu wa kuuwezesha zaidi Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu (CDF) ili kumudu vyema majukumu yake ya kusaidia uimarishaji wa zao la karafuu.

Alisema Mfuko huo unahitaji fedha nyingi hivyo imefika wakati kwa wadau ambao wameainishwa katika Sheria ya Maendeleo ya Karafuu namba 4 ya mwaka 2014 kuchangia mfuko huo wafanye hivyo ili kuuwezesha kutoa huduma za uimarishaji wa zao la karafuu.

Kwa mujibu wa sheria hiyo vyanzo vya mapato vya Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu ni mchango wa asilimia 1.5 ya mauzo ya karafuu nje ambapo ZSTC wanatakiwa kutoa, mchango wa asilimia 0.5 ya mauzo ya ndani ambapo wakulima wanatakiwa kutoa, faini za makoso yanayohusu zao la karafuu na mchango kutoka Serikali kuu.

Rate this item
(0 votes)

Contact Us
Why ZSTC?

We offer the best quality of Cloves in the market that has a strong taste and aroma. We offer the best price and it is negotiable.  Considering our terms of sales we do on-time shipment of your purchases. We provide free samples while attempting to try and purchase.

We're Open :0730 -1630Hrs EAT Mon-Friday
Sunday and Public Holidays: Closed