Hotline: (+255) 24-2230271 Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 

Sub Page Name

Usajili wa Wakulima na Wadau wa Zao la Karafuu

Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu umeanzishwa kwa Sheria Namba 2 ya mwaka 2014, chini ya kifungu nam. 4 (1), na kuzinduliwa rasmi tarehe 28/8/2015 na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Mfuko huu wa Maendeleo ya Karafuu upo chini ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC ambapo jukumu lake kubwa ni kuendeleza Sekta ya Zao la Karafuu.

Lengo kuu la Serikali kuanzisha Mfuko huu, ni kuhakikisha kuwa zao la karafuu ambalo ndio zao kuu la uchumi linaloipatia Zanzibar fedha nyingi za kigeni, linaendelezwa na linaenziwa kwa maslahi ya wakulima na wananchi wote.

Katika kulifikia lengo hili serikali imebuni mbinu na mikakati mbali mbali moja wapo ikiwemo kuwaenzi na kuwathamini Wakulima na Wadau wote wa zao la karafuu Zanzibar, kwa kuhakikisha wananufaika na juhudi zao za kilimo cha karafuu.

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu ambao upo chini ya Shirika la ZSTC imeamua kuwasajili wakulima na wadau wote pamoja na mashamba yao ya mikarafuu na mikarafuu yenyewe ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za uimarishaji wa zao la karafuu.

Kifungu nam. 10 (2) cha Sheria ya Maendeleo ya Karafuu Namba. 2 ya mwaka 2014 kinaweka wazi kuwa Kila mkulima wa karafuu, mmiliki, mkodishwaji, muuzaji au watu wengine wanaohusika na karafuu watapaswa kusajiliwa katika Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu.

Miongoni mwa faida kubwa kwa mkulima na mdau wa zao la karafuu kusajili ni kutambulika rasmi kuwa unajishughulisha za uimarishaji wa zao la karafuu ambapo utapatiwa kitambulisho maalum kitakachokurahisishia kupata huduma zinazotolewa na serikali katika uimarishaji wa zao la karafuu.

Kwa kujisajili Misaada inayotolewa na Serikali kama vile mikopo ya uchumaji, miche ya mikarafuu, majamvi ya kuanikia, bima kwa wachumaji wa karafuu wakati wanapopata ajali wakati wa uchumaji karafuu itawafikia wahusika moja kwa moja na kuepukana kuingia katika mikono ya wajanja wasiohusika na zao la karafuu.

Aidha, Serikali kupitia Shirika la ZSTC na Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi imekuwa na kawaida ya kutoa elimu kwa Wakulima wa zao la karafuu hivyo kwa kujisali wakulima watanufaika kirahisi na elimu inayotolewa.

Usajili utasaidia kujua idadi ya mashamba yote ya mikarafuu na mikarafuu yenyewe ambapo italiwezesha Shirika la ZSTC kufanya tathmini ya uzazi wa   karafuu kwa msimu ili kufanya maandalizi ya vifaa vinavyohitajika katika vuno na kujiandaa na       fedha za ununuzi.

Kutokana na kuwa zao la karafuu ni moja kati vyanzo vya mapato kwa Serikali usajili utaiwezesha Serikali kupanga vyema mipango ya maendeleo (bajeti) kutokana na mauzo ya karafuu nchi za nje na upatikanaji wa fedha za kigeni.

Usajili utapunguza au kuondosha kabisa tatizo la wizi wa karafuu mashambani na majumbani na ukataji wa mikarafuu unaofanywa na wezi wa karafuu kwa vile watu hao watakuwa hawana vitambulisho vitakavyowawezesha kuuza karafuu hizo.

“Fomu za usajili ni bure, kujisajili ni bure na kitambulisho kinapatikana bila malipo”

Shime wakulima na wadau wa zao la karafuu kuhimizane kujisajili wakulima na mashamba, kwa faida ya wakulima na kwa Maendeleo ya nchi.

 

 

Contact Us
Why ZSTC?

We offer the best quality of Cloves in the market that has a strong taste and aroma. We offer the best price and it is negotiable.  Considering our terms of sales we do on-time shipment of your purchases. We provide free samples while attempting to try and purchase.

We're Open :0730 -1630Hrs EAT Mon-Friday
Sunday and Public Holidays: Closed